Home Habari za michezo YANGA WAIJIBU SIMBA KWA KISHINDO….WASHUSHA MASHINE HII YA KAZI KUTOKA ULAYA…

YANGA WAIJIBU SIMBA KWA KISHINDO….WASHUSHA MASHINE HII YA KAZI KUTOKA ULAYA…

Habari za Yanga leo

Klabu ya Yanga imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Joseph Guédé Gnadou akiwa mchezaji huru baada ya kuachana klabu ya Tuzlaspor ya Uturuki.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tatu za mbele ikiwemo mshambuliaji wa kati na winga zote mbili anatumia mguu wa kulia.

Inaelezwa kuwa mashine hiyo ya kazi, imesaini mkataba wa miaka miwili, ambapo atakuwa akilipwa mshahara wa Dola 5500 sawa na Milioni 13.75 za kitanzania.

Usajili huo unaenda kuimarisha eneo la ushambuliaji la Yanga ikiwa ni matakwa ya kocha Miguel Gamondi baada ya kutokuwa na straika wa uhakika baada ya kutorishwa na kiwango cha waliokuwepo.

Gnadou ametua kuziba nafasi ya Hafiz Konikoni ambaye ametolewa kwa mkopo katika klabu ya Dogan Birlig ya Uturuki kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.

Awali Yanga ilikuwa imsajili mshambuliaji Ismail Auro Agoro raia wa Togo lakini kocha wao Miguel Gamondi akamkataa kufuatia staa huyo wa FAR Rabat kupoteza nafasi kwenye kikosi chake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPIGWA CHA 'UCHUNGU JUZI'...MPANGO WA SIMBA KWA WAARABU UKO HIVI...