Home Uncategorized MPANGO MKUBWA WA KUMALIZA LIGI KUU ENGLAND UPO NAMNA HII

MPANGO MKUBWA WA KUMALIZA LIGI KUU ENGLAND UPO NAMNA HII


IMEELEZWA kuwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England zimepanga kumalizia msimu wa 2019/20 kwa kucheza mechi zao zilizobaki bila kuwa na mashabiki na kwenye viwanja huru.

Mabosi wa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya England zimekubali kumalizia mechi 92 zilizobaki huku milango ya kuingilia mashabiki ikiwa imefungwa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Corona ambao ulianza mwezi Januari kusambaa kwa kasi.
Habari zinaeleza kuwa mpango huo utashirikisha mechi mbili ama tatu kwenye viwanja huru vya timu ambazo zinashiriki ligi lakini kwa muda tofauti.
Michuano ya EURO kwa 2020 imesimishwa kwa muda wa miezi 12 kuanzia Jumanne kutokana na Virusi vya Corona huku kwa upande wa Ligi Kuu England nayo pia kusimamishwa kwake kwa muda mpaka Aprili 3 kumewapa hofu wengi kuwa huenda itakuwa ngumu kumalizika kwa msimu huu.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAMOSI