Home Uncategorized CHAN NA AFCON KUPANGIWA TAREHE, KAMBI YA STARS YAVUNJWA

CHAN NA AFCON KUPANGIWA TAREHE, KAMBI YA STARS YAVUNJWA


MASHINDANO ya CHAN ambayo yanawashirikisha wachezaji wa ligi za ndani pamoja na yale ya Afcon yatapagiwa tarehe kulingana na hali itakavyokuwa ya ugonjwa wa Corona.

Dunia kwa sasa inapambana kutafuta kinga na dawa za virusi vya Corona ambavyo vimeanza kusambaa mwezi Januari nchini China.

 CAF imesitisha mashindano ya CHAN yaliyokua yafanyike Cameroon kuanzia Aprili 4-25,2020 mpaka pale hali ya ugonjwa wa Corona itakapotulia pia hata Afcon pia ilipaswa ifanyike nchini humo.

Taarifa ya CAF inasema imechukua hatua hiyo ili kulinda afya za Wachezaji,Viongozi,washirika na mashabiki. 


Timu ya Taifa ya Tanzania iliyo chini ya Etienne Ndayiragije ambayo ilikuwa imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya CHAN nayo imevunjwa.

SOMA NA HII  HILI HAPA JESHI KAMILI LA YANGA MSIMU WA 2020/21