Home Uncategorized HII HAPA SABABU YA MASTAA SIMBA KUPELEKWA MUHIMBILI

HII HAPA SABABU YA MASTAA SIMBA KUPELEKWA MUHIMBILI


 MASTAA wa Simba hivi karibuni walipelekwa Hospitali ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya moyo kabla ya mchezo wa Kariakoo Dabi.

 

Baadhi ya mastaa wa Simba ni Sadio Kanoute, Denis Kibu, Ousmane Sakho, Peter Michael na Henock Baka waliojiunga na timu hiyo hivi karibuni.

 

Simba na Yanga zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuvaana katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi hii.

 

Akizungumza na Championi JumatanoKaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwa wachezaji wao kufanyiwa vipimo vya moyo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.

 

Kamwaga alisema upo umuhimu mkubwa wa wachezaji wao kufanyiwa vipimo vya afya ikiwemo moyo ambao ni ugonjwa hatarishi kwa wachezaji.

 

Aliongeza kuwa, vipimo hivyo viliwahusisha wachezaji wote wapya na wa zamani pamoja na benchi la ufundi ili kujua afya zao.

 

“Kama Simba timu kubwa sisi tumekuwa na utaratibu wa kuangalia afya za wachezaji wetu kwa kuwafanyia kipimo cha ugonjwa wa moyo.

 

“Hivyo asubuhi wachezaji na benchi la ufundi wote walifanyiwa vipimo vya ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Muhimbili.

 

“Ugonjwa wa moyo unajulikana jinsi ulivyo hatarishi kwa wanamichezo, hivyo tumeona kuwafanyiwa mapema vipimo kabla ya kuanza kwa ligi,” alisema Kamwaga.

SOMA NA HII  REKODI YA GARETH BALE NDANI YA MADRID TAMU KINOMA