Home Habari za michezo HIZI HAPA REKODI ZA KUTISHA ZA WYDAD CA…SIMBA WAJIPANGE HASWAA!!

HIZI HAPA REKODI ZA KUTISHA ZA WYDAD CA…SIMBA WAJIPANGE HASWAA!!

HIZI HAPA REKODI ZA KUTISHA ZA WYDAD CA...SIMBA WAJIPANGE HASWAA!!

Wahenga walisema Kisiki cha Mpingo ni kigumu kuking’oa pengine kuliko aina yoyote ya mti.

Tunaweza kusema Simba Sc wamekutana na ‘Kisiki cha Mpingo’ hatua ya robo fainali ya Champions League.

Huo ndiyo ukomavu wenyewe, kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa hasa hatua ya robo fainali hutarajii kukutana na timu nyepesi.

Waydad Casablanca hawa ndiyo Mabingwa watetezi wa Kombe hili la CAF Champions League.

Waydad ni mara moja tu ndani ya miaka sita (6) ndiyo hawakuvuka hatua hii ya Robo Fainali ya CAFCL.

Ndani ya miaka sita (6), Waydad wamefika Fainali mara tatu na katika hizo 3 wamefanikiwa kuchukua Ubingwa mara mbili.
‘Simple’ tunaweza kusema Mnyama amekutana na ‘Kisiki cha Mpingo’ haking’oleki kwa Panga wala Shoka unahitaji Greda.

Rekodi za Wydad Casablanca CAF => 2023 yupo Robo Fainali => 2022 Bingwa Mtetezi na yupo Robo Fainali => 2021 Nusu Fainali => 2020 Nusu Fainali => 2019 Fainali (Mshindi wa Pili) => 2018 Robo Fainali 2017 Mabingwa

Rekodi za Simba Sc CAF => 2023 yupo Robo Fainali => 2022 Robo Fainali Shirikisho => 2021 Robo Fainali (Klabu Bingwa) => 2020 Walitolewa hatua ya awali => 2019 Robo Fainali => 2018 Hatua ya awali Kombe la Shirikisho => 2017 Haikushiriki.

SOMA NA HII  VIPERS vs SIMBA..DAKIKA 90 ZA WABRAZILI WAWILI KUAMUA HATMA ZAO...MMOJA HUENDA AKAFUKUZWA...