Home Habari za michezo DIARA AZIDI KUIPAISHA JUU LIGI YA TANZANIA…AITWA TENA MALI KWA KOMBE LA...

DIARA AZIDI KUIPAISHA JUU LIGI YA TANZANIA…AITWA TENA MALI KWA KOMBE LA DUNIA…


Kwa mara nyingine tena kipa wa Yanga, Djigui Diarra ameteuliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Mali ambacho kitacheza mechi mbili za hatua ya mwisho ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu dhidi ya Tunisia, Machi 25 na 29.

Kocha Mohamed Magassaouba amemjumuisha Diarra katika kikosi hicho cha wachezaji 28 ambacho kitakuwa na makipa watatu wakiwemo pia Ibrahim Mounkoro anayedakia TP Mazembe na Ismael Diawara wa Malmo ya Sweden.

Beki na nahodha wa timu hiyo, Hamari Traore wa Stade Rennes ya Ufaransa ataongoza jeshi hilo la nyota 28 lenye mastaa wengi wanaocheza soka la kulipwa katika ligi kubwa za soka barani Ulaya.

Abdoulaye Doucoure wa Everton, Yves Bissouma (Brighton), Moussa Djenepo (Southampton), Amadou Haidara (RB Leipzig) na Mamadou Fofana (Amiens) ni baadhi ya nyota wanaounda kikosi hicho cha Mali.

Nyota 28 wanaounda kikosi hicho ni makipa Mounkoro (TP Mazembe), Diawara (Malmo) na Diarra (Yanga), wakati mabeki ni Hamari Traore (Rennes), Mamadou Fofana (Amiens), Massadio Haidara (RC Lens), Amadou Dante (Sturm Graz), Boubacar Kouyate (Metz), Moussa Sissako (Standard Liege), Senou Coulibaly (Dijon), Almamy Traore (Eintracht Frankfurt) na Cheick Traore (Dijon).

Viungo ni Diadie Samassekou (TSG Hoffenheim), Mohamed Camara (RedBull Salzburg), Lassan Coulibaly (Salernitana), Aliou Dieng (Al Ahly), Amadou Haidara (RB Leipzig), Yves Bissouma (Brighton), Abdoulaye Doucoure (Everton) na Cheick Doucoure (RC Lens).

Upande wa washambuliaji kuna Moussa Djenepo (Southampton), Adama Traore (Sheriff Tiraspol), Moussa Doumbia (Reims), Abdoulaye Diaby (Al Jazira), Ibrahima Kone (Lorient), Ibrahima Sissoko (Niort), Nene Dorgeles (SV Ried) na Saliou Guindo (KF Laci).

Mali itacheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Tunisia, Machi 25 na zitarudiana huko Tunisia, Machi 29 na timu itakayopata matokeo mazuri katika mechi hizo mbili itafuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyika Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Disemba 18.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI WOTE KWA NINI KYOMBO ALITAMBULISHWA SINGIDA BIG STARS WAKATI ALISHASAINI MKATABA NA SIMBA...