Home Habari za michezo KUELEKEA LIGI YA MABINGWA MSIMU UJAO….CAF WAMUUMBUA MANARA…YANGA YAPANGWA KUANZA WALIPOISHIA …

KUELEKEA LIGI YA MABINGWA MSIMU UJAO….CAF WAMUUMBUA MANARA…YANGA YAPANGWA KUANZA WALIPOISHIA …


Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ leo Jumatatu (Juni 06) limethibitisha klabu ya Young Africans itaanzia hatau ya awali ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu ujao wa 2022/23. 

CAF imethibitisha uratibu huo, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuweka Video inayoonyesha Mshsamabuliaji wa klabu hiyo Fiston Mayele akiwasalimia mashabiki walipokua njiani. 

Young Africans itashiriki Michuano hiyo, kufuatia kuwa na uhakika wa kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, huku ikibakisha alama tatu kufikia lengo hilo. 

Katika hatua nyingine CAF imesisitiza klabu zote ambazo zitashiriki michuano ya Kimataifa kuhakikisha zinawasilisha mapema orodha ya majina ya wachezaji watakaosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo. 

Msimu uliopita Young Africans ilishiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini ilitolewa katika hatua ya awali kwa kufungwa jumla ya mabao 2-0 na Rivers United ya Nigeria. 

Taarifa hiyo ya CAF ni kama inamuumbua Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa kwa kitendo cha timu yake kutwa ubingwa msimu huu, basi moja kwa moja wataanzia hatua ya kwanza ya kufuzu michuano hiyo.

Msimu ujao Tanzania itawakilishwa na timu mbili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na mbili nyingine zitashiriki michuanio ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. 

SOMA NA HII  WAKATI AKIJUA TAYARI KASHAPONA..YANGA WAMPIGA STOP YACOUBA...APEWA SIKU 45...