Home Habari za michezo PABLO AKUBALI KUBEBA LAWAMA KIPIGO CHA SIMBA JANA…AFUNGUKA HALI ILIVYOKUWA NGUMU UGENINI…

PABLO AKUBALI KUBEBA LAWAMA KIPIGO CHA SIMBA JANA…AFUNGUKA HALI ILIVYOKUWA NGUMU UGENINI…


KOCHA mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema yuko tayari kubeba lawama kutokana na matokeo mabovu ambayo wameyavuna katika mchezo wa jana dhidi ya ASEC Mimosas.

Wekundu hao wa Msimbazi walikumbana na kichapo cha mabao 3-0 jana nchini Benin matokeo ambayo yamewafanya kuwa na hofu ya kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya Shirikisho Afrika licha ya kuwa na nafasi mpaka sasa.

Pablo amesema, anastaili kubeba lawama zote kwa kilichotokea lakini pia hata wachezaji wake wanapaswa kuhakikisha wanapambana sababu wanacheza timu kubwa.

“Hatukucheza vizuri, ni tofauti na matarajio yetu, kipindi cha kwanza ASEC walitawala mchezo na kupata mabao mawili cha pili tulirudi na tulipiteza nafasi za kufunga,” anasema Pablo huku akisisitiza vijana wake wanatakiwa kupambana zaidi ya jana katika mchezo wa mwisho.

Amesema kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwao kwa kuwa wenyeji wao walitawala huku akikiri makosa ya mchezaji mmoja mmoja na timu nzima kwa ujumla ndiyo yamepelekea matokeo hayo.

“Hatukucheza vizuri na kusababisha kupoteza mechi, kulikuwa na makosa na lazima yatugharimu hasa tukiwa ugenini,” amesisitiza Pablo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA AZAM FC...SIMBA SC WAIRAHISISHIA KAZI YANGA SC...