Home news SIRI NZITO YANGA…INJINIA HERSI ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA JINSI HALI ILIVYO…AMTAJA IBENGE…

SIRI NZITO YANGA…INJINIA HERSI ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA JINSI HALI ILIVYO…AMTAJA IBENGE…


YANGA imetoa tathimini ya mzunguko wao wa kwanza wa ligi lakini ndani yake yakatajwa mambo manne mazito yaliyoibeba timu hiyo huku mastaa Khalid Aucho na Yannick Bangala wakitajwa.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Mhandisi Hersi Said amesema kwamba mzunguko wa kwanza umeakisi mipango bora ya uwekezaji ndani ya kikosi chao.

Alisema mambo yaliyowabeba kwanza ni ubora wa wachezaji waliobaki na wapya waliosajiliwa katika kikosi chao msimu huu akisisitiza wengi wana ubora mkubwa kulinganisha na wengi wa timu nyingine.

“Timu hii tulianza kuijenga tangu misimu miwili iliyopita haikuwa kwa msimu mmoja ila kilichotokea msimu huu tuliboresha zaidi tukiwabakiza wachezaji wachache na kuongeza wengine bora zaidi, nafikiri hapa ndipo mafanikio ya msimu huu yalipoanza,” alisema Hersi ambaye alihusika kwa asilimia 100 katika usajili huo kupitia wadhamini wao GSM.

“Ukomavu ambao timu yetu umeonyesha ni mkubwa nimeona kuna takwimu mbalimbali za ligi katika mzunguko wa kwanza zimetolewa katika kila ubora Yanga tuko juu wengine wakifuatia, hiki ndicho ambacho klabu imelenga.

Jambo la pili ambalo Hersi alilitaja ni upana wa kikosi chao ambapo mbali na kuwakosa wachezaji wao wanane walio majeruhi lakini bado wengine waliweza kuziba nafasi zao.

“Kikosi chetu kina majeruhi wanane kwasasa, wengi hapo ni wale ambao walikuwa kikosi cha kwanza lakini kitu bora ni pale waliokuja kuziba nafasi zao hawakuonyesha tofauti kubwa, bado timu iliendelea kupata matokeo yaleyale ya ushindi au labda sare hii inaonyesha tulikuwa na daraja zuri la ubora kati ya wale wanaoanza na wanaokuja kuingia baadaye.

“Unaweza kuangalia mfano pale golini tukiamua kuanza na Diara (Djigui) kama chaguo la kwanza kipa aliyekuja kuingia badala yake ana mechi tano bila kuruhusu bao ambaye ni Mshery (Aboutwalib) ambaye ubora wake ni mkubwa.”

Hersi aliongeza kwamba jambo la tatu ni uwekezaji ambao waliufanya katika kikosi chao ambapo ukiacha mazingira bora ya kikosi chao kuishi pia walikuwa na maboresho makubwa ya posho mbalimbali kulingana na ugumu wa mchezo.

SOMA NA HII  SIMBA DAY YA MSIMU HUU USIPIMEEH...MABINGWA WA AFRIKA KUTUA NCHINI KUKIPIGA SIKU HIO

“Wachezaji walikuwa wanapambana sana kwasababu kuna kitu kikubwa wanajua wanakipata mchezo unapokwisha, posho zimekuwa zikijieleza, unajua kuna kile kiasi ambacho tumekuwa tukiwapa.

“Lakini inapokuja mechi ngumu kuna mambo yanabadilika, mfano ni mchezo wa Mtibwa Sugar tulipowatajia kiasi cha fedha ambacho tutawapa tulishtuka kumuona mtu kama Bangala (Yannick) akiwaambia wenzake kwa Kiswahili ‘jamani twendeni tukachukue fedha zetu’ wakati wakiwa wanaenda uwanjani.”

Aliongeza jambo la nne kuwa ni ubora wa kiungo wao Khalid Aucho na kiraka Bangala ambao wamekuwa na nguvu kubwa ndani ya kikosi chao cha kwanza msimu huu.

“Watu wanamuona Aucho juu ya ubora wake uwanjani ambacho ndio kikubwa lakini tulio ndani tunajua mambo bora zaidi ya hayo ya Aucho, akiwa mazoezini kuna wakati amekuwa akisimamisha mpaka mazoezi akiwahimiza wenzake kupambana kama anaona kasi ya mazoezi ni ndogo.

“Ukomavu wake umekuwa mpaka kwenye mechi amekuwa msaada mkubwa katika kuwaunganisha wenzake na kuongeza ubora na juu ya yote ubora wake mwenyewe umekuwa ujieleza huyu ni mchezaji mwenye thamani kubwa ambaye tulipambana kumleta hapa.

“Kuna Bangala nakumbuka wakati namsajili kocha Ibenge (Florent) aliniambia Yanga tumepata wachezaji bora wawili walio ndani ya mtu mmoja, tunapomkosa mtu pale nyuma anaweza kucheza kokote na ubora ukawa mkubwa, angalia pia akicheza katikati amekuwa kiraka mwenye ubora mkubwa.

“Mwisho ni umati wa mashabiki wetu wanatubeba sana,” alisema.