Home Uncategorized CHAMA: BWALYA ATATUBEBA KITAIFA NA KIMATAIFA

CHAMA: BWALYA ATATUBEBA KITAIFA NA KIMATAIFA

 


CLATOUS Chama, kiungo wa Simba  amesema kuwa kiungo mpya wa timu hiyo, Larry Bwalya atawabeba katika mechi za Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

 

Chama ameongeza kwamba kiungo huyo atakuwa msaada kwa Simba kutokana na kuwa na vitu vingi ambavyo atavitoa kwa klabu hiyo ikiwemo kufunga na kutengeneza mashambulizi.

 

Bwalya ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa ambapo Simba wamewasajili katika dirisha hili la usajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Power Dynamos ya Zambia.


Chama amehusika kuwashawishi mabosi wa timu hiyo wamsajili Bwalya amesema kwamba kiungo huyo ni msaada tosha ndani ya kikosi hicho na anaamini ataibeba timu hiyo kwenye michuano yote ambayo watashiriki.

 

“Ni mchezaji mzuri na naamini kabisa anakuja kuwa msaada mkubwa ndani ya timu na tutafanya vizuri katika michuano ambayo tutashiriki.

 

“Namjua na naamini kabisa atafanya vitu ambavyo vitatubeba katika mechi zetu za ligi lakini hata katika michuano ya kimataifa ambayo tutaenda kushiriki kwa baadaye,” alimaliza Mzambia huyo.

 

Bwalya ni miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Simba katika usajili wa dirisha kubwa.

 

Wengine ni Chris Mugalu, Joash Onyango, Ibrahim Ame, Charles Ilanfya, David Kameta ‘Duchu’ na Bernard Morrison.


Leo Agosti 22 Uwanja wa Mkapa ni kilele cha Simba day ambapo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki itakuwa dhidi ya Vital’O FC, ya Burundi lengo ikiwa ni kutoa burudani na kuwatambulisha wachezaji wapya.

SOMA NA HII  AZAM FC BADO WANALITAKA KOMBE HILI LILILOPO MIKONONI MWAO