Home Uncategorized AZAM FC BADO WANALITAKA KOMBE HILI LILILOPO MIKONONI MWAO

AZAM FC BADO WANALITAKA KOMBE HILI LILILOPO MIKONONI MWAO


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kazi kubwa nyingine iliyopo mkononi mwao ni kutetea taji lao la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mkononi mwao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa taji hilo lina umuhimu kwao kutokana na umuhimu wa mashindano hayo kwao.
“Sisi ni mabingwa watetezi jukumu letu ni kuona namna gani tutafikia malengo ambayo tumejiwekea, mashabiki watupe sapoti ili kufikia malengo,” amesema.

Hatua ya 32 bora kwa Azam FC itamenyana na Friends Rangers, Januari 27, atakayepenya hatua hiyo atatinga hatua ya 16.
SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YAANZA MAZOEZI RASMI