Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA ATEGUA MTEGO WAKE KIMTINDO

MBELGIJI WA SIMBA ATEGUA MTEGO WAKE KIMTINDO


SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ametugua  mtego wa dakika 180 kwa mechi mbili za kanda ya ziwa.
Simba imecheza mechi mbili ambazo ni sawa na dakika 180, Januari, 16 ilianza kushinda mabao 2-1 mbele ya Mbao FC  na mechi ya pili ya Januari 19 mbele ya Alliance FC ilishinda mabao 4-1 zote Uwanja wa CCM Kirumba.
Patrick Aussems alichemka kutegua mtego huo kutokana na matokeo ambayo aliyapata Aussems msimu uliopita wa 2018/19 ilipokutana na Mbao, Uwanja wa CCM Kirumba ilipoteza baada ya kucheza mechi zake tatu,msimu wa 2018/19 bila kufungwa.
Ushindi alioupata Sven umetegua mtego kwa kuwa alishinda mechi zote mbili na kurejea Bongo akiwa na pointi sita alizokusanya.

Kwa sasa, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 41 kibindoni, Sven amesema kuwa kikubwa ni wachezaji kuendelea kupambana kutafuta matokeo kwenye mechi zao zinazofuata.


SOMA NA HII  BERNARD MORRISON NA SHOMARI LAWI WANATUACHIA MASWALI MAGUMU