Home Uncategorized SIRI YA AZAM FC KUIPIGA MWADUI HII HAPA

SIRI YA AZAM FC KUIPIGA MWADUI HII HAPA

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kikubwa kilichowapa ushindi jana mbele ya Mwadui FC ni kujituma kwa wachezaji.

Azam FC jana ilishinda bao 1-0 mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Kambarage.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Shaban Chilunda dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Nicolaus Wadada.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa ushindi walioupata umetokana na wachezaji kujituma ndani ya uwanja pamoja na morali waliyokuwa nayo.

“Wachezaji wana morali kubwa na walipambana kutafuta matokeo ndani ya uwanja mwisho wa siku wakapata kile walichokuwa wanakihitaji,” amesema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA ASTON VILLA, SAMATTA KUFANYIWA VIPIMO KESHO