Home Uncategorized RASMI, SAMATTA AANZA MAZOEZI ASTON VILLA AKIANDIKA REKODI

RASMI, SAMATTA AANZA MAZOEZI ASTON VILLA AKIANDIKA REKODI

Mshambuliaji mpya wa Aston Villa, Mbwana Samatta ameanza rasmi mazoezi na kikosi chake kipya.

Samatta ameanza mazoezi na kuandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufanya kazi England akiwa na timu ya Premier League.

Villa imemsajili Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji kwa dau la pauni milioni 8.5 na kuandika rekodi mpya kwa soka ya Tanzania.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Mrisho Ngassa alifanya majaribio katika kikosi cha West Ham United chini ya Kocha Gianfranco Zola lakini hakufanikiwa.

SOMA NA HII  MAGORI: WIKI HII NI YA HATARI, WATU WATAZIMIA ZAIDI KWA USAJILI - VIDEO