Home Habari za michezo STAR SIMBA AFUNGUKA ISHU YA BALEKE KUPIGWA CHINI…” BORA TUSINGEMUACHA….”

STAR SIMBA AFUNGUKA ISHU YA BALEKE KUPIGWA CHINI…” BORA TUSINGEMUACHA….”

Habari za Simba SC

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Steven Mapunda ‘Garrincha’ ameukumbuka uwepo wa straika Jean Baleke ndani ya kikosi hicho, anaamini angekuwepo angekuwa na mabao mengi.

Baleke amejiunga na klabu ya Al lttihad ya Libya kwa mkopo kutoka TP Mazembe, huko anafunga, jambo lililomfanya Garrincha amkumbuke na kuona kwa sasa angekuwa kinara wa mabao kwa Ligi Kuu.

Baleke aliondoka Simba akiwa kinara wa mabao akifunga manane ambayo ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi bado hayajafikiwa, kwani Said Ntibanzokiza ‘Saido’ ana mabao saba.

“Kuna wakati mwingine najiuliza sipati jibu, kitu gani kiliwashawishi viongozi wa Simba kumuondoa Baleke? Waliopo wamechukua muda mrefu kufikia mabao yake, hilo liwatafakarisha viongozi,” amesema na kuongeza; “Kuna wakati mwingine mchezaji anaweza akapitia kwenye changamoto zinazohitaji hekima za viongozi kutatua na sio kumuondoa kwenye timu ilhali huduma yake bado inahitajika.

“Naamini Baleke angekuwepo hadi sasa angekuwa anaongoza kwa kufunga mabao mengi na huenda angekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.”

Ametolea mfano msimu uliopita akisema baada ya Simba kuukosa ubingwa, furaha ya mashabiki ilikuwa ni Saido kunyakua kiatu cha ufungaji bora alicholingana na Fiston Mayele kwa mabao 17.

Jambo jingine aliloushauri uongozi wa Simba ni kusaka kipa namba moja, kwa mtazamo wake anaona Aishi Manula kiwango chake kimeshuka.

“Ukweli usemwe, sina maana kwamba siheshimu mchango wa Manula, ila kwa sasa sifa ya kuitwa Stars na kuwa kipa namba moja wa Simba imepotea,” amesema.

SOMA NA HII  ALIKIBA AGOMEA KURUDI LIGI KUU BARA