Home Habari za michezo BAADA YA NAMUNGO KUFUNGWA JUZI…JULIO KAONA ISIWE TABU AISEE…KAFUNGUKA HAYA…AITAJA YANGA TENA…

BAADA YA NAMUNGO KUFUNGWA JUZI…JULIO KAONA ISIWE TABU AISEE…KAFUNGUKA HAYA…AITAJA YANGA TENA…


HUKU akieleza malengo yao ya kumaliza nafasi nne za juu bado yapo pale pale, Kocha Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amekubali kiroho safi kupoteza mechi kwa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, akisema ndiyo mpira na kuwapongeza wapinzani wao, akiahidi timu yake itafanya vema kwenye mechi zinazofuata.

Bao pekee kwenye mechi hiyo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mcha Hamisi ambalo lilitosha kuwafanya wenyeji kutoka uwanjani kifua mbele.

“Ukiondoa Yanga,  hakuna timu yoyote kwenye ligi hii ambayo haijafungwa, mpira ni mchezo wa makosa, mpira umepigwa umemgonga mchezaji wangu kwenye mkono ikawa penalti, basi goli limefungwa, lakini vijana wangu wamecheza vizuri, hatukuweza kutumia nafasi hasa kipindi cha kwanza.

“Kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri, kipindi cha pili tukacheza vizuri sana, lakini wenzetu walituachia tumiliki mpira, nadhani kwa sababu walikuwa tayari wana bao, wameshinda tunawapongeza na huu ni mpira, bado mechi nne, azma yetu iko pale pale kushika nafasi ya nne au ya tatu,” alisema Julio.

Naye Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji, Mohamed Muya, alisema malengo yao ya kushinda mechi hiyo yametimia.

“Malengo yetu leo (juzi) ni kushinda, tunashukuru vijana wamepambana, tumepata bao moja, sasa tunayo matuimaini ya kubakisha timu Ligi Kuu, mapambano yanaendelea,” alisema kocha huyo.

Wakati Namungo ikisalia na pointi zake 37, Dodoma Jiji imefikisha jumla ya pointi 31, ikiwa kwenye nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 msimu huu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA USHINDI WA JUZI....MAKI KATAZAMA MASTAA WAKE WEEH....KISHA AKATIKISA KICHWA KUKATAA UWEZO WAO...