Home Habari za michezo KISA GOLI LA BIASHARA UTD JUZI….MABEKI YANGA KUKIONA CHA MOTO…KAZE AAPA ‘KULALA...

KISA GOLI LA BIASHARA UTD JUZI….MABEKI YANGA KUKIONA CHA MOTO…KAZE AAPA ‘KULALA NAO MBELE.’…


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema atakaa na mabeki wake kufanya tathmini ya bao walilofungwa kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara juzi dhidi ya Biashara United, akidai kuwa ni jepesi na ambalo lilipaswa kufungwa kwenye mechi za mchangani za watoto na si Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza baada ya mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Kaze raia wa Burundi alisema mabeki wake walifanya makosa makubwa, kwani wakati goli linafungwa kulikuwa na mabeki wawili tu ndani ya boksi.

“Haiwezekani tumeshafunga bao, halafu wanatufunga goli kwenye ndani ya boksi, na tupo wawili tu, ni makosa makubwa sana, tunapaswa kukaa na kutathmini hili. Bao kama hili wanafungwa watoto kwenye mechi za mchangani na si kwa timu kubwa kama Yanga na kwenye Ligi Kuu,” alisema Kaze.

Lilikuwa ni bao la Mkenya Collin Opare dakika ya 77, akiunganisha krosi iliyochongwa na Mkenya mwenzake, Ambrose Awio, ikiwa ni dakika tatu tu baada ya Yanga kupata bao lililofungwa na Fiston Mayele, timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.

Akizungumzia mechi hiyo, Kaze alisema wangeweza kupata mabao matatu kipindi cha kwanza kama si umakini mdogo wa wachezaji wake.

“Naweza kusema tungeweza kushinda tangu mwanzo, tumepoteza nafasi tatu za kufunga, mechi za hivi ukishindwa kufunga mpaka mapumziko, unampatia nguvu ya kuzuia mpinzani, lakini tumepokea pointi moja, tumecheza na timu ambayo imetupatia ushindani mkubwa, tunaangalia mechi inayofuata,” alisema.

Mrundi mwenzake Kocha Mkuu wa Biashara United, Vivier Bahati alisema kwa asilimia kubwa wachezaji wake walicheza kwa kufuata maelekezo, japo kuna wakati waliteleza na ndipo walipoadhibiwa.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AMPA MTIHANI HUU NGOMA