Home Habari za michezo KISA SARE YA 2-2 DAR…WAKONGWE WAIBUKA NA HILI KWA ROBERTINHO NA SIMBA...

KISA SARE YA 2-2 DAR…WAKONGWE WAIBUKA NA HILI KWA ROBERTINHO NA SIMBA YEKE…

Habari za Simba

BAADA ya Simba kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Al ahly katika mchezo wa kwanza mashindano ya African Football League, wakongwe wa soka nchini wametoa mbinu za kufanya katika mchezo wa marudiano.

Pia wamezungumzia makosa waliyoyaona upande wa Simba katika mechi na kushauri nini kifanyike ugenini.

Beki wa zamani wa Yanga, Kenneth Mkapa alisema mastaa wa Simba walikuwa dhaifu kimwili na kila walipoporwa mpira walikosa nguvu ya kupambana ili kuurejesha mikononi mwao.

Alisema shida nyingine kubwa ilikuwa safu ya ulinzi kwani haikuwa katika ubora na ndio maana iliruhusu mabao mepesi.

“Simba wanatakiwa kuwa na mawasiliano kwani kuna wakati walifungwa kutokana na walinzi kushindwa kusogea kwa haraka ili kuzuia,” alisema Mkapa.€

Pia alisema na kushauri: “Huwezi kutengeneza nafasi za kufunga kama timu haina ushirikiano kwani kila mtu anafanya anachoweza na sio anachotakiwa.”€

Kiungo wa zamani wa Simba, Dua Said alisema matokeo ya mchezo wa juzi hayakupatikana kwa sababu Ahly ni timu kubwa, lakini ukosefu wa umakini kwa wachezaji.

Alisema wakati beki kama Shomari Kapombe anachukua mpira kukabwa, nyuma yake kunakuwa hakuna mtu anayesimama kusaidia.

“Wanapokwenda ugenini wazingatie zaidi kucheza na sio kuhofia timu kubwa kwani Simba wanawaweza kabisa (Waarabu) ila tu umakini ulikosekana,” alisema.€

“Al Ahly hawakufunga mabao ya kushangaza, walifunga kawaida ila kwa sababu wanajua nini wanataka na hawana hofu wanacheza kwa ushirikiano. Kama ukichukua mpira kwao basi watahamia kumkaba aliye nao mpaka waupate.”

Naye Adolf Rishard alisema bao la Kibu Dennis lilikuwa bora na Kanoute alifunga la mazoezini likimaanisha kwamba alielewa na kuwa tayari kupambana.

Alisema wachezaji wanatakiwa kuwa kama Kibu kuwa na hisia za kufunga wakati wote ili waweze kuipa timu mafanikio. “Ugenini wakacheze kama walivyofanya Al Ahly hapa, walicheza kwa utulivu mkubwa. Kocha aongeze viungo wengi wa kati ili waweze kuzuia kila mashambulizi,” alisema.

“Hawatakiwi kuwaachia nafasi nyingi washambulie eneo la kati lijae ili kuweza kujenga uzito wa wapinzani kusogelea lango lao.”

Simba ilitarajiwa kuondoka jana kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa keshokutwa katika Uwanja wa Cairo International.

SOMA NA HII  TUKIO LA MANULA KUTOKWA DAMU MKONONI GHAFLA KABLA YA MECHI YA JANA...ISHU NZIMA KUMBE IKO HIVI...SHABIKI ATAJAWA..