Home Uncategorized EXCLUSIVE: YANGA YAMALIZANA NA KIFAA KIPYAA!!

EXCLUSIVE: YANGA YAMALIZANA NA KIFAA KIPYAA!!


Klabu ya Yanga imemalizana rasmi na Mlinda Mlango aliyekuwa anaichezea Mbao FC, Metacha Mnata.

Usajili huo umekuja baada ya makubaliano ya pande zote mbili kati ya mchezaji na klabu.


Mnata alianza kuhusishwa kutua Yanga kwa muda mrefu na hatimaye usajili wake umekamilika rasmi.

Kinachosubiriwa hivi sasa ni kipa huyo kuungana na wachezaji wenzake huko Morogoro ambapo kikosi kimeweka kambi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Ujio wa Mnata Yanga utamfanya achukue rasmi nafasi ya Klaus Kindoki ambaye inaelezwa ataachwa huku namba mbili ikishikiliwa na Ramadhan Kabwili.

SOMA NA HII  TAIFA STARS YAMWEKA NJIA PANDA TANASHA