Home Habari za michezo MAYELE ATUPA JIWE LA GIZANI SIMBA….AFUNGUKA KINACHOMSIBU NA TIMU YAKE YA MISRI….

MAYELE ATUPA JIWE LA GIZANI SIMBA….AFUNGUKA KINACHOMSIBU NA TIMU YAKE YA MISRI….

Habari za Michezo

Straika wa zamani wa Yanga Fiston Mayele akizunguzia ubora wa timu yake ya zamani Yanga kuwa unazidi kupanda Kila Siku mwaka Jana wao walicheza fainali lakini Sasa hivi wameingia makundi baada ya miaka 25 kwahiyo ni hatua kubwa.

Lakini wakati akiwa anazungumzia ubora wa chama lake la zamani ametupa kijembe kwa wapinzani wake Simba kwamba wamebebwa na kanuni timu inaingia makundi na haijamfunga mwenzie wamefuzu kwa kanuni.

“Yanga inakua Kila Siku wanacheza na wanakupa burudani,Simba kwanza wameingia hatua ya makundi kwa goli la ugenini we uliona wapi hoyo?.Amesema Fiston Mayele mshambuliaji wa Zamani wa Yanga.

Katika hatua nyingine Mayele amesema ni suala la muda tu kabla hajaanza kutetema vilivyo kwenye ligi Kuu ya Misri kama alivyokuwa akifanya Tanzania,.

Baada ya kucheza michezo mitatu ya Ligi na miwili ya Ligi ya Mabingwa pasipo kufunga bao lolote.

Fiston Mayele ametoa neno kwa wale wote wanaomsema kuhusiana na kuanza kwake na ukame wa mabao katika Klabu ya Pyramid FC.

“Ligi hapa ni ngumu kiasi, lakini haitachukua Muda nitaanza kuwanyesha namna nzuri ya kutetema kama kawaida yangu”.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA....BOSI SportPesa AIBUKA NA HAYA....ADAI WALIFURAHI KUACHANA NAO...