Home Uncategorized SABABU YA AZAM FC KUPOTEZA LEO MBELE YA KCCA HII HAPA

SABABU YA AZAM FC KUPOTEZA LEO MBELE YA KCCA HII HAPA


KOCHA msaidizi wa timu ya Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wamepoteza mchezo wa leo kutokana na mchanganyiko wa wachezaji wapya na wazamani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa haina tatizo kupoteza mchezo wa leo mbele ya KCCA kwa kufungwa bao 1-0 kwani ni sehemu ya mchezo.

“Tumepambana ila haikuwa bahati yetu kwani wachezaji wetu bado wana mchanganyiko kuna wale wapya na wazamani hivyo muda si mrefu tutakuwa bora, mchezo wetu unaofuata tutapambana kushinda,” amesema.

Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Kagame wanaiwakilisha Tanzania wakiwa na KMC, mchezo wa kwanza walishinda bao 1-0 mbele ya Mukura FC.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA WATAJA SABABU YA KUKAZA NDANI YA LIGI KUU BARA