Home Uncategorized BREAKING: KOTEI ASEPA SIMBA MAZIMA, APIGWA PINI MIAKA MITATU

BREAKING: KOTEI ASEPA SIMBA MAZIMA, APIGWA PINI MIAKA MITATU


TIMU ya Kaizer Chiefs imemsajili James Agyekum Kotei kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, amejiunga na Kaizer akitokea Simba SC.
Usajili wa Kotei ndani ya kikosi hicho, unamaanisha kwamba Willard Katsande atatakiwa kujipanga kisawasawa kutetea nafasi yake.

Kotei ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Kaizer baada ya wiki hii mshambuliaji raia wa Zambia, Lazarous Kambole kujiunga na timu hiyo.

Nyota kadhaa wa kikosi hicho wameachana na timu hiyo msimu uliomalizika hivi karibuni akiwemo Ryan Moon, Hendrick Ekstein, Bhongolethu Jayiya‚ Gustavo Paez na Virgil Vries.
Kocha wa kikosi hicho,Ernst Middendorp, yupo kwenye mikakati ya kukisuka upya kikosi hicho kuelekea msimu ujao.

SOMA NA HII  MBWANA SAMATTA KUWASILI BONGO KESHO