Home Uncategorized TAIFA STARS: KESHO LAZIMA KIELEWEKE MBELE YA KENYA

TAIFA STARS: KESHO LAZIMA KIELEWEKE MBELE YA KENYA


BEKI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Gadiel Michael amesema kuwa kwa sasa wana nafasi ya kupata matokeo chanya mbele ya Kenya mchezo wa pili kwenye michuano ya Afcon nchini Misri.

Tanzania na Kenya wote wameanza vibaya michuano ya Afcon baada ya kupoteza michezo yao ya ufunguzi ambapo Tanzania ilifungwa mabao 2-0 na Senegal huku Kenya ikipoteza mbele ya Algeria kwa kufungwa mabao 2-0.


“Mchezo wa kwanza kwetu ulikuwa mgumu licha ya kupambana ila kwa sasa tayari tumefanyia kazi makosa yetu lazima tupambane mbele ya Kenya kesho ili kupata matokeo,” amesema Michael.

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufuzu kushiriki michuano ya Afcon baada ya kufanya hivyo miaka 39 iliyopita.

SOMA NA HII  ISHU YA MABADILIKO, SIMBA YAKUBALI KUFUATA TARATIBU ZA SERIKALI