Home Uncategorized NDANDA YATOSHANA NGUVU NA SIMBA NANGWANDA

NDANDA YATOSHANA NGUVU NA SIMBA NANGWANDA


KIKOSI cha Ndanda leo kimelazimisha sare ya bila kufungana na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Mchezo wa leo Ndanda iliyo chini ya Kocha Mkuu, Meja Mstaafu, Abdul Mingange iliingia uwanjani kwa tahadhari kubwa ikisaka ushindi ili kuweza kujinusuru kwenye hatari ya kushuka daraja.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck haikuwa na cha kupoteza kwa kuwa tayari wameshatangazwa kuwa mabingwa.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 2-0 ila leo mambo yamekuwa magumu kwa Ndanda kulipa kisasi na kufanya wagawane pointi mojamoja.

Ndanda inafikisha jumla ya pointi 37 huku Simba ikifikisha jumla ya pointi 80 kibindoni.

SOMA NA HII  WAGOSI WA KAYA NAO HAWAKO NYUMA WAANZA HIVI KWENYE DIRISHA DOGO LA USAJILI