Home Uncategorized TAKUKURU YABAINISHA KINACHOENDELEA ISHU YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI KWA AJILI YA...

TAKUKURU YABAINISHA KINACHOENDELEA ISHU YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI KWA AJILI YA AFCON


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), jana ilimuita ofisini kwao Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za maandalizi ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana ‘Afcon U17’.
Takukuru jana ilianza mahojiano hayo na Kidao kwa ajili ya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha hizo zilizotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Afcon U17 yaliyofanyika mwaka jana hapa.
Kabla ya mahojiano kuanza, Takukuru ilisema kuwa kama kuna mtu yeyote anahusika na matumizi mabaya ya shilingi bilioni moja ambayo ilitolewa na Rais kwa ajili ya mashindano hayo arudishe.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Takukuru, Doreen Kapwani alithibitisha kwa Kidao kufika ofisini kwao jana asubuhi kwa ajili ya mahojiano maalum na maofisa wa taasisi hiyo.

Kapwani alisema kuwa katibu huyo ndiyo wa kwanza kuitwa kuhojiwa huku msururu mwingine wa maofisa wa TFF wakitarajiwa kuripoti wakati wowote ofisini kwao.

Aliongeza kuwa Takukuru tayari wameanza uchambuzi wa baadhi za nyaraka kutoka kwenye shirikisho hilo ili kujua matumizi ya fedha hizo jinsi zilivyotumika.
 “Nikuthibitishie tu kuwa Kidao yupo tangu asubuhi na amefika hapa leo (jana), kwa ajili ya mahojiano juu ya kashfa ya ufujaji wa fedha za Afcon (U17).
“Fedha hizo zilitolewa na Rais (Magufuli) kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana ya Afrika (Afcon 17), ambayo yalifanyika hapa nchini, mwaka wa jana.
“Hivyo, leo (jana) tumeanza na Kidao ambaye ni katibu baada ya huyu kumaliza kuhojiwa, maofisa wengine wa TFF watafuatia kwa ajili ya mahojiano kwani tayari tumeanza uchambuzi wa nyaraka mbalimbali kutoka TFF,” alisema Kapwani.
SOMA NA HII  SIMBA WAONGOZA KIKOSI CHAO KUITWA TWIGA STARS - VIDEO