Home Uncategorized SIMBA YATAJA SABABU YA MECHI ZAO 10 KUWA NGUMU

SIMBA YATAJA SABABU YA MECHI ZAO 10 KUWA NGUMU


JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa wana kazi kubwa ya kupambana kwenye mechi 10 kutokana na wapinzani wao kujipanga kupata matokeo.

Simba imecheza mechi 28 za Ligi Kuu Bara kibindoni imejikusanyia pointi 71 na imefunga mabao 63 na imefungwa jumla ya mabao 15.

Ligi Kuu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13 baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo ambayo yalisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Bocco amesema:”Tuna kazi ngumu na kubwa kupambana kutafuta matokeo kwani mechi zetu nyingi zina ushindani mkubwa, ukizingatia kwamba kila timu inajua inahitaji nini.

“Timu ambazo zinashuka ni nyingi nasi tunatakiwa tupambane ili kushinda haitakuwa kazi rahisi lakini tunaamini kwamba kwa kuwa tumeanza mazoezi basi tutafanya kazi,” amesema.

Simba ilianza mazoezi Mei 27 baada ya wachezaji kuripoti kambini rasmi.

SOMA NA HII  MWANTIKA AREJESHWA TAIFA STARS