Home Uncategorized GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA

GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA


INJINIA Hersi Said,Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM amesema kuwa mpango mkubwa wa kuwa wadhamini ndani ya Klabu ya Yanga ni kuona kwamba siku watakayoondoka wanaacha alama ndani ya Yanga.

Hayo ameyazungumza leo kwenye ukumbi wa Serena kwenye hafla ya utiliaji saini kati ya Yanga, La Liga na GSM kuelekea safari ya mabadiliko ambapo mgeni rasmi ni Rais mstaafu wa awamu ya nne.Jakaya Kikwete.

 “Tuna historia ya wadhamini wengi wa Yanga ambao waliwekeza kwa muda siku walipoondoka Yanga iliyumba, sisi hatuna mpango huo tunataka siku tutakayoondoka tuache alama ndani ya Yanga, tuache thamani ili Yanga isimame kwa miguu yake miwili.

“Pia La Liga, kupitia Klabu ya Sevilla ya Hispania ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kupitia utalii, mafanikio makubwa klabu yetu itapata iwapo tutaweza kushirikiana nao vizuri tutapata nafasi kubwa sana ya kuitangaza nchi yetu,” amesema. 

Tayari mkataba wa kuanza safari ya kuelekea kwenye safari ya mabadiliko umeshasainiwa ambapo Mshindo Msolla ambaye ni Mwenyekiti kwa niaba ya Yanga na Injinia.Hersi Said kwa niaba ya GSM.

SOMA NA HII  YANGA YATOA TAMKO KUHUSU KUJIUZULU KWA VIONGOZI WAO PAMOJA NA WALE WALIOJIENGUA