Home Habari za michezo KUHUSU HATMA YA KAGERE MSIMBAZI KWA MSIMU UJAO….AHMED ALLY AFUNGUKA NAMNA MAKUBALIANO...

KUHUSU HATMA YA KAGERE MSIMBAZI KWA MSIMU UJAO….AHMED ALLY AFUNGUKA NAMNA MAKUBALIANO YALIVYO…


Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema straika wao Meddie Kagere bado ana mkataba na Wekundu hao hivyo ataendelea kuwepo.

Ahmed amesema, Kifaru huyo wa Rwanda bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na ndio maana ameambatana na kikosi kilichoondoka leo nchini kuelekea Misri.

“Kagere bado yupo kwa mwaka Zaidi ndani ya Simba. Hivyo tutakuwa naye kwa msimu unaokuja,” alisema Ahmed.

Simba wameondoka nchini leo Julai 14, 2022 kuelekea Misri ambapo watakaa pre season kwa takriban wiki tatu kisha kurejea nchini kuanza msimu mpya wa 2022-23.

SOMA NA HII  'FEI TOTO' AFUNGUKA MAJUKUMU YAKE MAPYA YANGA...AWATAJA WACHEZAJI WENZAKE...