Home Habari za michezo IMEVUJA RASMI…KIPA KINDA SIMBA AWEKEWA ULINZI MZITO…ISHU KAMILI A-Z HII HAPA

IMEVUJA RASMI…KIPA KINDA SIMBA AWEKEWA ULINZI MZITO…ISHU KAMILI A-Z HII HAPA

IMEVUJA RASMI...KIPA KINDA SIMBA AWEKEWA ULINZI MZITO...ISHU KAMILI A-Z HII HAPA

Kila mchezaji wa Simba alikuwa anajaribu kumlinda Ally Salim Juma kiakili na kimwili ili aendelee kuwepo kwenye mchezo.

Utaona kila alipokuwa akifanya jambo zuri karibu wachezaji wote walikuwa wanaenda kumuonesha wapo pamoja nae na kile anachokifanya wanakithamini.

Ingetokea wanamfokea/kumkaripia pale alipofanya makosa inawezekana angehisi yupo golini lakini wachezaji wazoefu hawamuamini.

Lakini uwepo wa Ally Salim golini uliongeza umakini kwa wachezaji wengine kwa sababu wanatambua golikipa wao si mzoefu wa mechi za aina ile kwa hiyo jukumu lao ni kuhakikisha hafikiwi na purukushani nyingi na kama itatokea anafikiwa basi iwe hakuna namna ya kuzuia.

Mazingira ya aina hiyo ameshakutananayo Manyika Jr, Kabwili na jana ilikuwa kwa Ally Salim.

Timu nzima inakuwa makini kwa sababu wanajua kuna mtu sio mzoefu wa mechi kubwa.

SOMA NA HII  UCHAGUZI MKUU YANGA: MANARA ATANGAZA 'SAPRAIZI' KUBWA KWA MASHABIKI....UKUMBI MZIMA WALIPUKA KWA SHANGWE....