Home Habari za michezo WABABE WA YANGA WATUA DAR KIBABE…WAPANIA KUPIGA KWENYE MSHONO….

WABABE WA YANGA WATUA DAR KIBABE…WAPANIA KUPIGA KWENYE MSHONO….

Tetesi za Usajili Yanga

Ihefu FC mzuka umepanda kwani baada ya ushindi katika mechi iliyopita, imeanza kusuka mipango upya kuimaliza tena Yanga huku benchi la ufundi likitoa msimamo katika duru hili la lala salama.

Ihefu haikuwa na mwanzo mzuri lakini kwa sasa imeonekana kuimarika baada ya kuichakaza KMC bao 1-0 kwenye mechi iliyopita na sasa kituo kinachofuata ni Dar es Salaam kuwavaa Yanga, Januari 14 mwaka huu.

Timu hiyo ya mkoani hapa ndiyo inashikilia rekodi ya kuisimamisha Yanga ambayo ilikuwa imecheza mechi 49 bila kupoteza kabla ya kuitibulia rekodi kwa kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Highland Estate, wilayani Mbarali.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Zuberi Katwila alisema matokeo waliyonayo hivi sasa yamewapa mwanga katika kupambana kukwepa rungu la kushuka daraja na bado hawajapoa.

Alisema hesabu za sasa ni kusuka mipango upya kuhakikisha wanaendeleza rekodi msimu huu kuwanyoosha Yanga akibainisha kuwa mechi zilizobaki katika raundi hii hawaachi kitu.

“Pamoja na matokeo yetu yanayovutia hivi sasa, lakini tunajua bado kazi ni ngumu inahitaji nguvu ya ziada kusaka ushindi kwenye mechi zilizobaki, tunatengeneza mikakati kushinda tena mchezo ujao dhidi ya Yanga,” alisema Katwila.

Nahodha wa timu hiyo, Joseph Mahundi alisema bado hawapo sehemu nzuri hivyo wanahitaji ushindi zaidi ili kujikwamua kutoka nafasi za chini na kufufua matumaini ya kumaliza ligi salama.

“Nafasi ya 13 tuliyopo kwa pointi 20 si rafiki sana, tunahitaji umoja na mshikamano huu uendelee kwenye mechi zilizobaki na kumaliza pazuri kwenye ligi, tuko tayari kwa mapambano, tunaomba sapoti ya mashabiki,” alisema Mahundi.

SOMA NA HII  USAJILI WOTE ULIOKAMALIKA BONGO HUU HAPA....ISHU YA BALEKE NA PHIRI BADO NGUMU...