Home Uncategorized VUGUVUVUGU LA MACHI 8 LAWAZIBA MDOMO SIMBA

VUGUVUVUGU LA MACHI 8 LAWAZIBA MDOMO SIMBA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuelekea Machi 8 hautakuwa na maneno mengi zaidi ya kuwataka mashabiki wakutane uwanjani kuongea kwa vitendo.

Machi 8 kutakuwa na pambano la watani wa jadi litakalowakutanisha Yanga na Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Simba inakumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye pambano la kwanza lililopigwa Januari 4 Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:-“Tunaziba kabisa mdomo kuhusu hiyo Machi nane, hapana kikubwa zaidi ya kusema tukutane uwanjani,”.

SOMA NA HII  DU SANCHEZ NOMA ANAKUNJA MKWANJA MREFU BALAA, UWANJANI NAKO BALAA