Home Uncategorized RUVU SHOOTING: WAO WANA PIRA BIRIANI SISI TUNA PIRA KAVUKAVU

RUVU SHOOTING: WAO WANA PIRA BIRIANI SISI TUNA PIRA KAVUKAVU


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba utakaochezwa Oktoba 26, Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.


Bwire amesema kuwa kwa kuwa Simba wanatamba na sera yao ya pira biriani wao wanakuja na pira kavukavu ndani ya uwanja na wana imani ya kupata pointi tatu jumlajumla.


Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa wengi wanasahau kwamba kuna timu inaitwa Ruvu Shooting na inacheza mpira wa pasi nyingi mithili ya Barcelona jambo litakalowapa tabu wapinzani wao Simba.


“Maandalizi yapo vizuri, unapozungumzia Ruvu ujue unazungumzia timu yenye mpira wa pasi nyingi mithili ya Barcelona sasa tunakwenda kukutana na Simba kazi itakuwa ndani ya uwanja.


“Huwa wanatusahau tukiwa tunacheza na timu nyingine na kutazama tunacheza na nani hatuiangalii Simba tu tunacheza na timu zote ambazo zipo kwenye ligi.

“Utapigwa mpira mkubwa uwanjani zaidi ya ule ambao wamechezewa kule walikotoka. Nimepokea simu nyingi sana nikipewa matokeo yao nami pia nimeona hivyo acha tu wafungwe kwani mpira una matokeo mengi ndani ya uwanja.

“Kilichobaki kwetu ni kuona namna ambavyo tutacheza na kufanya vizuri ndani ya uwanja, wao wana mpira biriani sisi ni pira kavukavu mwanzo mwisho,” amesema.

SOMA NA HII  TEGETE AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI