Home Uncategorized OKTOBA 26 SIMBA KAZINI TENA

OKTOBA 26 SIMBA KAZINI TENA

 

KIKOSI cha Simba kina kibarua kingine tena Oktoba 26 kumenyana na timu ya Ruvu Shooting ambayo nayo ni mwendo wa kijeshi ndani ya uwanja kama ilivyo Tanzania Prisons.

Simba wakiwa wametoka kuchezeshwa ligwaride na Tanzania Prisons Oktoba 22 Uwanja wa Nelson Mandela kwa kufungwa bao 1-0 wana kazi nyingine ya kufanya Uwanja wa Uhuru.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroek amesema kuwa matokeo ambayo waliyapata nyuma ni sehemu ya mchezo hivyo watafanyia kazi makosa yao.
SOMA NA HII  VIDEO: WABRAZIL WA SIMBA BADO KUNA KAZI, ILA KWA YANGA BALAMA AKIPEWA NAFASI ATAPETA