Home Uncategorized MINZIRO: TUPO KWENYE NAFASI MBAYA, NIMEWANOA WACHEZAJI KUIMALIZA COASTAL UNION

MINZIRO: TUPO KWENYE NAFASI MBAYA, NIMEWANOA WACHEZAJI KUIMALIZA COASTAL UNION

Habari za Michezo leo


KOCHA Mkuu wa Mbao FC, Felix Minziro amesema kuwa amewanoa wachezaji wake vizuri kuelekea kwenye mchezo wao utakaocheza dhidi ya Coastal Union Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10:00.

Minziro amesema kuwa  kikosi chake kipo kwenye nafasi mbaya kwa sasa hivyo lazima wapambane kupata matokeo kujinasua hapo walipo.

“Tupo kwenye nafasi mbaya hivyo nimewaambia wachezaji wangu lazima tupambane kupata matokeo mazuri ili kujitoa hapa tulipo kwa sasa.

“Nimewanoa na kuwanoa wachezaji ili kuwa fiti, mpira una mambo mengi hilo ninalijua hivyo mashabiki wasichoke kutupa sapoti,” amesema.

Mbao FC ipo nafasi ya 19 baada ya kucheza mechi 30 kibindoni ina pointi 23 inakutana na Coastal Union ikiwa nafasi ya tano na pointi 48 iliyo chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda.

SOMA NA HII  BENZEMA AHUSISHWA NA UGAIDI KUFUATIA SAKATA PALESTINA