Home Uncategorized MANCHESTER CITY WATEMBEZA MKONO KWA BURNEY

MANCHESTER CITY WATEMBEZA MKONO KWA BURNEY


PHIL Forden, nyota wa Manchester City alifungua pazia la ushindi wa mabao 5-0 mbele ya kikosi cha Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana na kufunga pia.

Alianza kufunga dakika ya 22 kisha Riyad Mahrez alipachika mabao mawili dakika ya 43 na 45 kwa mkwaju wa penalti na lile la nne likapachikwa na David Silva dakika ya 51 kabla ya Forden kufunga pazia la mabao dakika ya 63.

City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Pep Guardiola ni Mabingwa watetezi na hesabu zao kubwa ni kushinda mechi zote ili kuweza kutwaa taji hilo msimu huu.

Wapinzani wao wakubwa ni Liverpool ambao wapo nafasi ya Kwanza, wakiwa wamecheza jumla ya mechi 30 na pointi 83 huku City ikiwa na pointi 63. Burnley wao wapo nafasi ya 11 na pointi zao ni 39.

SOMA NA HII  ALLY MAYAY AKANUSHA TAARIFA ZA KUICHANA YANGA 'SIYO MIMI JAMANI'