Home Uncategorized ZANA KUSAINI MIAKA MIWILI SIMBA

ZANA KUSAINI MIAKA MIWILI SIMBA


Imeelezwa kuwa beki wa klabu ya Simba, Zana Coulibaly yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu ya Simba.

Taarifa imesema kuwa Zana anaweza akasaini mkataba wa miaka miwili tayari kuendelea kuhudumu mpaka mwaka 2021.

Coulibaly alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miezi sita katika dirisha dogo la ligi kuu Bara December mwaka jana mkataba ambao umeisha June 15.

Mchezaji huyo ambaye yupo likizo hivi sasa anatarajiwa kurejea Tanzania tayari kukamilisha dili hilo siku yoyote kuanzia leo.

SOMA NA HII  ZAHERA AIZUNGUMZIA MECHI YA SIMBA VS UD SONGO ' MIMI SIJUI' - VIDEO