Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MAYELE KUTAKIWA VIPERS….UKWELI WA JAMBO NI HUU…

KUHUSU ISHU YA MAYELE KUTAKIWA VIPERS….UKWELI WA JAMBO NI HUU…

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers, Alex Isabirye ametolea ufafanuzi juu ya timu hiyo kuhusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Kalala Mayele.

Akizungumza kutoka Kampala Uganda, Isabirye amesema hakuna kocha asiyependa kufanya kazi na mchezaji kama Mayele kutokana na ubora alionao kwenye mashindano ya ndani na nje lakini sio jambo rahisi kihivyo na hawana pumzi ya kumng’oa kwenye klabu yake ya sasa Yanga SC

“Kwa sasa ni nani ambaye hajui ubora wa Mayele? Binafsi sidhani hata klabu yake iko tayari kumuacha mchezaji kama yeye kwenye kikosi chao kutokana na alivyoisaidia na kuipa mafanikio hadikufika hapa ilipo,” amesema Isabirye.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIFUNGIA TANZANIA GOLI JUZI...GEORGE MPOLE "AMPIGA BITI" KOCHA TAIFA STARS...AMPA SHARTI HILI....