Home Uncategorized MTIBWA SUGAR: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

MTIBWA SUGAR: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa leo utambana mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa jambo ambalo linawafanya na wao wapambane kwenda sawa na kasi iliyopo.
“Tunatambua kwa sasa mambo bado hayajawa mazuri, tumetoka kulazimisha sare na Namungo uwanja wa nyumbani sio mbaya bado tuna nafasi ya kukazana na kurejea kwenye ubora wetu.
“Wachezaji wanaumia na matokeo mabaovu hata ssi pia hatupendi lakini mchezo wa mpira una matokeo matatu tunajipanga na tupo tayati kwa mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar,” amesema.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI