Home Uncategorized HAPA NDIPO YANGA ILIPOIPOTEZA SIMBA JUMLAJUMLA

HAPA NDIPO YANGA ILIPOIPOTEZA SIMBA JUMLAJUMLA


KWENYE misimu 11 ya hivi karibuni ambapo Yanga na Simba wamekutana Yanga inashikilia rekodi ya kupindua meza kibabe.

 mechi 23 walizokutana Yanga imeshinda mechi sita, Simba saba na kutoa sare mechi 10 rekodi zinaonyesha kuwa ni mechi nane timu ilitoka nyuma ikiwa imefungwa bao na kupindua meza kwa kuweka mzani sawa na kugawana pointi mojamoja.
Yanga inaongoza kupindua meza ikiwa imetoka nyuma mara tano huku Simba ikifuatia ikitoka nyuma mara tatu na kugawana pointi mojamoja na mpinzani wake ipo namna hii:-
Msimu wa 2008/2009 ,Aprili 19 Simba 2-2 Yanga, Yanga ilianza kufungwa na Simba kupitia kwa Ramadhan Chombo dk 23 likasawazishwa na Ben Mwalala dk ya 48 na bao la pili lilifungwa na Haruna Mosh dk ya 62 likasawazishwa na Jerry Tegete dk ya 90.
 Msimu wa 2012/13, Oktoba 3, Yanga 1-1 Simba, Simba ilianza kufunga dk ya 3  na Amri Kiemba  na Yanga ilipindua meza kupitia kwa Said Bahanuzi dk ya 65.
Msimu wa 2013/14. Aprili 19, Yanga 1-1 Simba, Simba ilianza kufunga dakika ya 76 kupitia kwa Haruna Chanongo lilipinduliwa na Simon Msuva dk ya 86.
Msimu wa 2017/18 ,Oktoba 28, Yanga 1-1 Simba, Simba ilianza kufunga dk ya 58 kupitia kwa Shiza Kichuya lilipinduliwa na Obrey Chirwa dk ya 60.
Msimu wa 2019/20, Januari 4,2020, Simba 2-2 Yanga, Simba ilianza kufunga kupitia kwa Meddie Kagere dk ya 42 na Deo Kanda dk ya 46, Yanga ilipindua kupitia kwa Mapinduzi Balama dk ya 49 na Mohamed Issa dk ya 52.
Simba pia wamo walipindua meza kibabe msimu wa 2010/11, Machi 5  kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Yanga ilianza kufunga dk ya 59 kupitia kwa Stephan Mwasyika lilipinduliwa na Mussa Mgosi dk ya 73.
2013/14 Oktoba 20, Yanga 3-3, Yanga ilianza kufunga mabao kipindi cha kwanza kupitia kwa Mrisho Ngassa dk 15,Hamiss Kiiza dk ya 35 na 45 Simba ilipindua kupitia kwa Betram Mombeki dk ya 54, Joseph Owino dk ya 58 na Gilbert Kaze dk ya 85.
Msimu wa 2016/17,  Oktoba Mosi, Simba 1-1 Yanga, Yanga ilianza kufunga kupitia kwa Amiss Tambwe dk ya 26 lilipinduliwa na Shiza Kichuya dk ya 87.
SOMA NA HII  KISA CORONA, BEKI SIMBA AJIFUNGIA NDANI AKICHEZA GEMU