Home Habar za Usajili Simba KUHUSU ISHU YA KAGERE KUTEMWA SIMBA….WAKALA WAKE ASHINDWA KUVUMILIA…AIBUKA NA HOJA HIZI...

KUHUSU ISHU YA KAGERE KUTEMWA SIMBA….WAKALA WAKE ASHINDWA KUVUMILIA…AIBUKA NA HOJA HIZI NZITO..


Meneja wa Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Medie Kagere, amavunja ukimya na kumkingia kifua mchezjai wake, anayehusishwa na mpango wa kuondoka Simba SC.

Kagere anatajwa kuwa kwenye mpango wa kuachwa Simba SC, kwa kuzingatia kiwango chake msimu uliopita, ambapo hakufanya vizuri kama ilivyokua kwa misimu miwili ya awali alipotua Msimbazi.

Hata hivyo Meneja wa Mshambuliaji Patrick Gakumba amegeuza upepo na kusema kuwa, Mchezaji wake ataendelea kuwa sehemu ya Kikosi cha Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania Bara kwa msimu ujao.

Gakumba amesema Kagere bado ana mazingira mazuri ya kuendelea kucheza soka Simba SC, na msimu ujao atakua na makali zaidi kutoka na wachezaji wanaosajiliwa klabuni hapo, kuwa na uwezo wa kumchezesha na kufunga mabao.

Kuhusu umri wa Mshambuliaji huyo, Meneja huyo ambaye pia ni Raia wa Rwanda amesema, Umri ni namba na hadhani kama ni jambo sahihi linalopaswa kutumika kumuhukumu mchezaji wake.

“Watasubiri sana, Kagere haondoki Simba, Medie Kagere ni mchezaji mzuri, pamoja na kwamba umri umeenda lakini hilo sio tatizo, age is just a number”

“Msimu uliopita timu ilikuwa mbovu, sio kwamba Kagere kiwango kilishuka,, Kikubwa watengeneze timu tu” amesema Patrick Gakumba

Kagere alisajiliwa Simba SC msimu wa 2019/20 akitokea Gor Mahia ya Kenya, akicheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara alifunga mabao 23 na msimu uliofuata 2020/21 alifunga mabao 22.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA KAZIKAZI HAINA KUPOA