Home Uncategorized YANGA YAZIDI KUNG’ARA KIMATAIFA, YAINGIA DILI NONO NA KAZIER CHIEFS

YANGA YAZIDI KUNG’ARA KIMATAIFA, YAINGIA DILI NONO NA KAZIER CHIEFS


MABINGWA wa kihistoria Tanzania, Yanga wameanzisha ushirikiano na klabu kubwa ya Kaizer Chiefs, vinara wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Hiyo ikiwa ni miezi michache imepita tangu Yanga iingie udhamini na wadhamini wao ambao ni Kampuni ya GSM Tanzania chini ya Said Gharib Mohamed ambaye ni Rais wa Makampuni ya GSM.

GSM hadi hivi sasa imeifanyia makubwa klabu hiyo kubwa na kongwe nchini ikiwemo kufanikisha usajili wa wachezaji watano katika usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Wachezaji hao ni kiungo fundi Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Muivory Coast Yikpe Gnaimen, Tariq Seif, Adeyum Salem na Ditram Nchimbi huku ikifanikisha kumshusha kocha mpya wa timu hiyo Luc Eymael aliyetua jana.

Yanga kupitia wadhamini wao, Kampuni ya GSM, walipata mwaliko kutoka Chiefs kwenye sherehe ya kutimiza miaka 50 ya klabu hiyo tangu ianzishwe nchini huko Afrika Kusini.

Katika sherehe hizo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, ndiye aliyehudhuria tafrija hizo huku akipata nafasi ya kutoa zawadi ya jezi ya Yanga yenye chata ya GSM kwa baadhi ya viongozi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa kupitia kwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alithibitisha hilo kwa kusema kuwa: “Ni kweli Hersi alipata mwaliko huo kutoka Chiefs katika sherehe ya kutimiza miaka 50 ya klabu hiyo.

“Mengi wamezungumza na viongozi wa Chiefs na kikubwa ni kujenga ushirikiano kati ya klabu hizi mbili kwenye masuala mbalimbali ya soka kati ya Yanga na Chiefs.”
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA