Home Uncategorized NONDO WA COASTAL UNION AWAKUBALI MABEKI HAWA BONGO

NONDO WA COASTAL UNION AWAKUBALI MABEKI HAWA BONGO


BEKI chipukizi wa Coastal Union, Bakari Nondo amesema kuwa amekuwa akivutiwa na uwezo wa wazawa wanaokipiga ndani ya Simba na Yanga kutokana na uwezo wao.

Ukuta wa Coastal Union umekuwa imara msimu huu ambapo kwenye mechi 28 ilizocheza na pointi 46 imefungwa mabao 19.

“Ninajifunza kwa wenzangu ambao ninakubali kazi zao wakiwa ndani ya uwanja, kwa upande wa mabeki ambao ninakubali kazi zao kwa Bongo ni pamoja na Kelvin Yondani na Erasto Nyoni hawa wapo vizuri.

“Wamekuwa wakinipa ushauri na kunionyesha njia ya kufanya kufikia mafanikio, nina amini kazi bado ipo kufika mbali zaidi ya hapa,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU KUFUTWA KWA LIGI KUU BARA