Home news USAJILI WA MCHEZAJI WA KICONGO WAIPONZA SIMBA…FIFA YAINGILIA KATI..UONGOZI WATOA TAMKO..

USAJILI WA MCHEZAJI WA KICONGO WAIPONZA SIMBA…FIFA YAINGILIA KATI..UONGOZI WATOA TAMKO..


SIKU chache baada ya Fifa, kuiamuru Simba imlipe straika Mkongomani, Doxa Gikanji, Million 110 uongozi wa timu hiyo umeibuka na kukiri kuwa ni kweli wamepokea taarifa hizo watazifanyia kazi.

Fifa imeiamuru Simba kufanya hivyo baada ya kuvunja mkataba wa mchezaji huyo, walimsajili Januari 2021 lakini walishindwa kumsajili dirisha la CAF, Agosti 2021 wakaamua kuvunja naye mkataba na ndipo mchezaji huyo alienda Fifa kulalamika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alithibitisha kupata taarifa hiyo na kusisitiza kuwa wataifanyia kazi kwasasa hawezi kuzungumza chochote hadi bodi itakapokaa na kuamua nini watakifanya.

“Ni kweli mchezaji huyo tulifanya naye mazungumzo na kumtumia mkataba lengo lilikuwa ni kumtumia kwenye mashindano ya kimataifa kipindi tulipofika hatua ya makundi klabu bingwa Afrika,” alisema na kuongeza kuwa.

“Hatukuweza kukamilisha usajili wake kwenye mashindano hayo ndio maana hakuonekana kwenye kikosi cha Simba tumeshtuka kuona faini hiyo sitaweza kuwa na jibu la moja kwa moja kwamba tutalipa ni lazima tukutane na kujadili hili,” alisema.

Mbali na deni hilo waliloamuliwa kulipa Simba pia wapo kwenye kesi ya kutakiwa kulipa milioni 294 kwa kosa la kukiuka usajili wa winga wao wa zamani, Shiza Kichuya.

Simba ililimwa fedha hizo baada ya klabu ya Pharco FC ya Misri kulalamikia kitendo cha timu hiyo kumsainina na kumtumia Kichuya akiwa na mkataba uliotokana na dili walilofanya mwaka juzi.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA: TUTAWAFUNGA VITA