Home Simba SC KOCHA SIMBA: TUTAWAFUNGA VITA

KOCHA SIMBA: TUTAWAFUNGA VITA


KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes ametamba kuwa anaamini kikosi chake kitaweza kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.

Simba wanatarajia kuwa wenyeji wa AS Vita ya DR Congo katika mchezo wa tano wa kundi A utakaopigwa Jumamosi ya Aprili 3, huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Februari 12, nchini DR Congo.

Mpaka sasa Simba ndiyo vinara wa msimamo wa kundi A la michuano hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 10, wakifuatiwa na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Al Ahly wenye pointi saba, AS Vita wao wako kwenye nafasi ya tatu na pointi zao nne huku Al Merrikh ya Sudani wao wakiburuza mkia na pointi yao moja.

“Tunajua tuna mchezo mgumu mbele yetu dhidi ya AS Vita, lakini nina imani kubwa vijana wangu watapambana ili kuweza kupata pointi tatu muhimu hapa nyumbani.” amesema Gomes.

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA 'KUBUTULIWA' MOROCCO...MBRAZILI SIMBA APEWA 'KONGOLE'....