Home kimataifa USHINDI WA MABAO 14 WA TIMU YA TAIFA JAPAN WAWEKA REKODI

USHINDI WA MABAO 14 WA TIMU YA TAIFA JAPAN WAWEKA REKODI



TIMU ya Taifa ya Japan, imeweka rekodi ya kupata ushindi mkubwa ambao haujawahi kutokea ndani ya dakika 90 katika harakati za kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Ushindi wa mabao 14-0 dhidi ya Mongolia walioupata Jumanne ya Machi 30 unawafanya wawe kwenye rekodi hiyo tamu huku wakiwa na nafasi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya 7. Walikuwa hawajacheza tangu Novemba 2019 kutokana na janga la Virusi vya Corona. 

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Fuku-Ari dakika 90 wapinzani wa Japan walikamilisha bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango huku Japan ikipiga jumla ya mashuti 25 ambayo yalilenga lango la wapinzani hao 

Matokeo hayo yanaifanya Japan kuwa nafasi ya kwanza katika kundi F na pointi zao ni 15 baada ya kucheza mechi 5 huku Mongolia ikiwa nafasi ya tano na pointi zao ni 3 baada ya kucheza mechi 7.

Mshambuliaji wa Southampton ambaye yupo huko kwa mkopo akitokea Klabu ya Liverpool, Takumi Minamino alifungulia mvua ya mabao dk 13 kwenye mchezo huo.

Kazi ikaendela kupitia kwa Yuya Osako alipiga hat trick dk ya 23,55 na 90+2, Daichi Kamada dk 26, Hidemasa Morita dk 33, Knash-Erdene Tuyaa alijifunga dk 39, Sho Inagaki alitupia mawili dk 68,90+3, Junya Ito alitupia mawili dk 73 na 79, Kyongo Furuhashi pia alitupia mawili dk ya 78 na 86 pamoja na Takuma Asano dk 90+1.


SOMA NA HII  ARTETA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUONGEZA KUJIAMINI