Home Azam FC JAMA JAMA ..HAWA AZAM FC HAWATAKI MZAHA MSIMU HUU….WAMESHUSHA KOCHA LINGINE LA...

JAMA JAMA ..HAWA AZAM FC HAWATAKI MZAHA MSIMU HUU….WAMESHUSHA KOCHA LINGINE LA KUTISHA…ALIKUWA FC PORTO…


Klabu ya Azam imemtambulisha rasmi, Joao Rodrigues raia wa Ureno kuwa mtaalamu wao mpya wa tiba za wachezaji (physiotherapist).

Rodrigues ametua usiku wa kuamkia leo Jumamosi ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kinachotaka kufanya vizuri msimu huu.

Rodrigues ni mtaalamu wa viwango vya juu kwenye tiba za wachezaji, akiwahi pia kufanya kazi na mabingwa wa Ureno, FC Porto.

Mmiliki wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa kabla ya kuanza msimu huu aliahidi atawapa furaha mashabiki wake kwa kuleta wachezaji wa hali ya juu, kocha wa viungo, kocha wa makipa na sasa amemaliza kwa kushusha ‘physio’ wa viwango.

Baada ya ujio wake sasa benchi la ufundi la timu hiyo litakuwa chini ya Kocha wake Mkuu, Abdihamid Moallin, Omary Nasser, ambaye ni Msaidizi, kocha wa washambuliaji, Kali Ongala, kocha wa viungo, Mikel Guillen na kocha wa makipa, Dani Cadena.

SOMA NA HII  BAADA YA KUBEBA TUZO YA Ballon D'Or JUZI...BENZEMA ATAJA TIMU ATAKAYOSTAAFIA SOKA...