Home Uncategorized KAZE: NAKUJA YANGA KUFANYA KAZI, AFUNGUKA KILICHOMCHELEWESHA

KAZE: NAKUJA YANGA KUFANYA KAZI, AFUNGUKA KILICHOMCHELEWESHA

  


CEDRIC Kaze,amesema kuwa leo anaweza kutua rasmi Bongo kumalizana na Yanga ili aanze kufanya kazi yake mpya kwa kuwa matatizo yake ya kifamilia ameshayaweka sawa.


Awali Kaze ilipaswa aje Bongo Agosti 25 kukinoa kikosi cha Yanga akichukua mikoba ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi ilishindikana kwa kuwa aliweka bayana kwamba anahitaji muda wa wiki mbili kutatua matatizo ya kifamilia.


Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Yanga ulimshusha Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ambaye alidumu kwa muda wa siku 36 na kufutwa kazi Oktoba 3 baada ya kumaliza mchezo wake wa tano aliousimamia dhidi ya Coastal Union.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa ilikuwa ngumu kuwahi kufika Bongo kutokana na masuala ya kukamilisha safari yake kwa kuwa yupo ugenini jambo ambalo limechukua muda kidogo.


 “Huku kwa wenzetu Canada ni tofauti na sehemu nyingine hasa ukizingatia kwamba nipo ugenini, suala kubwa lipo kwenye kukamilisha masuala ya usafiri ukizingatia kwamba nipo na familia jambo ambalo limechukua muda kidogo.

“Napenda kuwaambia mashabiki wa Yanga kwamba Alhamisi usiku nitakuwa Tanzania na mambo yakienda sawa basi nitakamilisha masuala yangu na uongozi wa Yanga kwani nimekuwa nikiwasiliana nao muda mrefu.


“Uwezo ninao na ninaitambua Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na nimeifuatilia kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita, ukitazama ina wachezaji wengi wazuri na wana kikosi kizuri hivyo matarajio yangu ni kuona timu inaingia kwenye ushindani na inafanya vizuri.”

Kaze ana historia nzuri na soka la Ulaya kufuatia kuwahi kufundisha Akademi ya FC Barcelona, anatarajia kutua nchini kukisimamia kikosi cha Yanga kuweza kutimiza ndoto yake ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu mitatu mfululizo.


Kwa sasa Yanga imecheza mechi tano za ligi ikiwa na pointi 13 na kibindoni imefunga mabao saba huku ikiwa imefungwa bao moja.

SOMA NA HII  SHIKALO ATANGAZA SIKU YA KUTUA YANGA