Home Habari za michezo PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO…SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI…ZAGOMBANIWA...

PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO…SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI…ZAGOMBANIWA KWA NJUGU….

Licha ya jezi za Yanga kutawala kuelekea mchezo wa timu hiyo dhidi ya Coastal Union leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa jijini Arusha, jezi za Simba zimeoneoka kuzipiga bao kwa bei.

Sasa kuelekea mchezo huo jezi za Yanga ndizo zimeonekana kutawala sana nje ya uwanja huo lakini zikipigwa bao na za watani zao Simba ambazo licha ya uchache lakini bei yake hazishikiki.

Jezi za Yanga mpya zinauzwa bei tofauti zile za njano na kijani ni Sh35000 ambayo ni bei elekezi huku nyeusi zikiuzwa Sh50,000 wakati jezi mpya za Simba zinauzwa Sh60,000.

Mmoja wa wauza jezi uwanjani hapo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema jezi za Simba ndio zinauzika zaidi kwa kufuatiwa na za Yanga lakini pia chache za Coastal Union ambazo zipo uwanjani hapo.

“Unajua jezi za Yanga zimetoka nyingi tofauti na Simba hivyo  hata bei yake siyo kubwa sana lakini kama hapa unaona ya Simba ni moja tu lazima mtu atanunua kwa garama yoyote.” amesema.

SOMA NA HII  SAMATTA NA 'BATAGOAL' WAIPA SIMBA MCHONGO WA MAANA..UKITIKI HUO NI WATAKUWA 'MUSWANO'