Home news SAMATTA NA ‘BATAGOAL’ WAIPA SIMBA MCHONGO WA MAANA..UKITIKI HUO NI WATAKUWA ‘MUSWANO’

SAMATTA NA ‘BATAGOAL’ WAIPA SIMBA MCHONGO WA MAANA..UKITIKI HUO NI WATAKUWA ‘MUSWANO’


MABINGWA mara nne mfululizo, Simba kufikia sasa msimu huu wamefunga mabao nane tu katika mechi nane, wastani wa bao moja kwa mechi, jambo ambalo limewastua wadau ambao wamewapa mchongo Wekundu hao ili kuirejeshea timu makali yake ili ibebe ndoo ya tano msimu huu.

Licha ya kuongezeka kwa ushindani kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na mkwanja mrefu wa udhamini wa haki za televisheni uliomwagwa na Azam Media na kuzipa nguvu timu nyingi, Simba bado inaweza kutisha kwa kiwango cha juu kama mambo kadhaa yatafanyika, amesema straika wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Emmanuel Gabriel ‘Batigol’.

Mabao nane waliyofunga Simba yanalingana na timu ya Mbeya Kwanza inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani na licha ya kuwa na mechi moja pungufu, bado wastani wa bao moja kwa mechi kwa Simba ni jambo la kutupiwa jicho hasa kutokana na ubora ambao Wekundu hao wameonyesha katika miaka ya karibuni kwa kutoa vipigo vizito.

Gabriel amesema wachezaji wengi wa Simba wana uchovu kutokana na kutumika ndani ya miaka minne mfululizo ambayo walichukua ubingwa.

Alisema msimu ulioisha namba tatu za juu za wafungaji zilishikiliwa na washambuliaji wa Simba, John Bocco (16), Chris Mugalu (15) na Meddie Kagere (14) ambaye alikuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara.

“Kagere anaonekana anakiwasha kwasababu hakutumika sana msimu ulioisha, Bocco akipata mapumziko na mwili wake ukajijenga kwa ajili ya kazi atawashangaza wengi,” alisema Gabriel na akaongeza kuwa;

“Kama Simba watasajili basi waongeze straika mwingine wa kuwapa changamoto Kagere na Bocco maana nimesikia Mugalu ana majeraha,” alisema.

Mchezaji mwingine wa zamani wa timu hiyo, Ally Pazi Samatta, baba wa Mbwana Samatta alisema bado Simba ina kikosi kizuri ila wachezaji wamechoka maana asilimia kubwa wametumika sana ndani ya misimu minne.

“Kocha ajue tu namna ya kuwatumia, watatisha tena.”

SOMA NA HII  KOCHA AL AHLY ALALAMIKA WAPITA NJIA KAMA ZA SIMBA