Home Burudani KOCHA AL AHLY ALALAMIKA WAPITA NJIA KAMA ZA SIMBA

KOCHA AL AHLY ALALAMIKA WAPITA NJIA KAMA ZA SIMBA

Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Marcel Koller, alia na mfululizo wa mechi huku akiitaja ratiba kuwa kikwazo kwa timu yake kupata matokeo mazuri hasa kwenye michuano mipya ya African Football League inayotarajiwa kuzinduliwa Dar es Salaam.

Koller ameyasema hayo siku chache kabla ya mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa AFL dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, akisistiza kuwa wachezaji wake wametumika sana hivyo anahofia wanaweza wasimpe anachokitaka kwenye mchezo huo.

Amekumbusha kuwa kwenye mazingira kama hayo walijikuta wakipoteza taji la African Super Cup.

“Ratiba zinapangwa bila kuwajali wachezaji, kwenye mazingira kama haya sijui tutarajie nini. Inajulikana kabisa ni masaa mengi kusafiri ndani ya bara la Afrika, bado itategemea wachezaji wangu watakuwa kwenye mazingira gani baada ya kutua Tanzania, hapo ndio tutajua tutacheza vipi.”

SOMA NA HII  AHMED ALLY AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU VIINGILIO VYA SIMBA DAY MAMBO HADHARANI